Kumekua na mapigano makali ya kurushiana risasi na
silaha nzito nzito katika mji wa Bangui nchini Jamuhuri ya Afrika ya
Kati saa moja kabla Baraza kuu la Umoja wa Mataifa halijapitisha azimio
la kupeleka majeshi ya kutoka Afrika na Ufaransa.
Mwandishi wa habari wa BBC aliyepo katika mji wa
Bangui anasema ameona magari ya kivita yakiendeshwa yakipita katika
mitaa na kwamba watu wengi bado wamejifungia majumbani mwao.Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa Gerald Araud ameiambia BBC kuwa kuongezwa majeshi ya kimataifa utasaidia hali ya usalama ndani ya wiki chache..
Bwana Araud amesema Majeshi ya Umoja wa Afrika na yale ya Umoja wa Mataifa yanapaswa kusimamia sheria na utulivu katika mji wa Bangui kabla ya kuangalia usalama katika miji mingine nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
0 comments:
Post a Comment