Pages

ETOILE;SIMBA MCHUKUWENI TU OKWI SISI HATUWEZI KUMLIPA.



WAKATI straika Emmanuel Okwi akiwa Dar es Salaam, timu yake ya Etoile du Sahel imeendelea kufulia na kuitaka Simba imchukue mchezaji huyo ili mambo yaishe juu kwa juu.

Simba iliipa Etoile du Sahel mpaka Septemba 30 mwaka huu iwe imelipa Sh 480 milioni za kumnunua mchezaji huyo, lakini hilo halijafanyika mpaka sasa.

Wiki iliyopita, Simba iliandika barua kwenda kwa uongozi wa Etoile du Sahel, lakini timu hiyo ya Tunisia haijajibu lolote.



“Jamaa wana hali mbaya kiuchumi, wanatulazimisha tumchukue Okwi, halafu watulipe fedha kidogo kama fidia, lakini bado sisi hatuafiki tunasubiri mpaka hiyo Septemba 30. Wakishindwa tunakwenda moja kwa moja Fifa,” alisema mmoja ya viongozi wa Simba jana Jumatatu.

“Okwi mwenyewe yupo tayari kurudi Simba wakati wowote, lakini ngoja kwanza tusubiri hiyo Septemba 30 ambayo ndio siku ya mwisho tuliyokubaliana na Etoile du Sahel,” alisema.

Okwi mwenyewe ambaye yupo Dar es Salaam aliliambia Mwanaspoti jana Jumatatu kuwa amekuja nchini kwa mapumziko mafupi na kutuliza akili yake.

Akiwa Dar es Salaam, Okwi amekuwa akitumia gari aina ya Subaru yenye rangi nyekundu kwa ajili ya kufanya mizunguko yake.

Tangu atue katikati ya wiki iliyopita alikuwa akiishi katika Hoteli ya Sapphire, Kariakoo na mashabiki wa soka walimshuhudia kwenye mechi ya Simba na Mbeya City Jumamosi iliyopita katika sare 2-2 kwenye Uwanja wa Taifa.

Mwanaspoti ilizungumza na Okwi na mahojiano yalikuwa hivi.

Swali: Vipi, Okwi ujio wako Dar es Salaam unaashiria nini?

Jibu: Nipo kwa ajili ya mambo yangu binafsi na zaidi ni mapumziko tu, nategemea kuondoka Jumatano (kesho) kurudi Uganda.

Swali: Ni mambo gani hayo binafsi au unafanya mazungumzo na Simba kwa ajili ya kurudi?

0 comments:

Post a Comment