Pages

KATI YA EMANUEL OKWI NA TAMBWE HAMIS NANI MKALI?soma sifa zao ndani.




GUMZO la Jiji la Dar es Salaam kwa sasa ni makali ya straika wa Simba, Tambwe Hamis. Simba inajisifu kwa kusajili mastraika wakali na wenye uchu wa kuzitikisa nyavu ingawa Azam FC inatamba kutwaa tuzo za ufungaji Bora wa Ligi Kuu Bara.

Katika misimu mitatu ya ligi iliyopita, Azam imeandika rekodi ya kutoa wafungaji bora wa ligi mfululizo. Nyota waliotwaa tuzo wakiwa Azam ni Mrisho Ngassa ambaye amerejea Yanga, John Bocco na Kipre Tchetche.

Kwa Simba imekuwa na historia nzuri kusajili mastraika wenye uchu na kiwango kizuri cha kuchana nyavu za timu pinzani.

Baada ya kutimka kwa Emmanuel Okwi Januari mwaka huu na kutua Klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia. Safu ya upachikaji mabao ya Simba ilipotea na kuigharimu timu hiyo na kushindwa kutetea taji la ubingwa wa ligi hiyo na kujikuta ikimaliza nafasi ya tatu kwa tabu.

Kwa sasa Simba imempa Amis Tambwe mkataba wa miaka miwili afanye kazi na ameonyesha makali tangu kuanza kwa ligi.

Sifa za Tambwe

Tambwe kimo chake hakifiki futi sita ingawa ana kiwango kizuri kuruka juu na kupachika mabao ya vichwa. Pia, wepesi wake na ujanja wa kucheza na maeneo ya kufunga ni moja kati ya siri yake kubwa ya kufunga kila mara. Vilevile ni mtulivu na mwenye kufanya uamuzi wa haraka kuliko kawaida haswa kwenye mashuti.

Anatumia akili zaidi kila anachokifanya kuliko nguvu.

Straika huyo ambaye hucheza na Betram Mwombeki kwenye fowadi ya Simba, amecheza mechi nne za ligi dhidi ya Oljoro JKT, Mtibwa Sugar, Mgambo JKT na Mbeya City.

Katika mechi hizo amefunga mabao sita na kushika usukani wa orodha ya wafungaji. Kwa kifupi anajua kufunga.

Udhaifu wake

Kimo chake hakifiki futi sita. Kuna wakati anakutana na mabeki warefu na kumpa wakati mgumu kufunga na kutimiza wajibu wake uwanjani. Hana pilikapilika nyingi wala hauwezi mpira wa mabavu.

0 comments:

Post a Comment