Maji taka yamezagaa katika kambi ya Umoja wa mataifa ya wakimbizi Sudan Kusini
Umoja wa mataifa Nchini Sudan
Kusini umejitetea vikali kutokana na ukosoaji kwamba inawabagua watu
wanaotaabika ndani ya makao yake makuu katika jiji kuu la Sudan Kusini
Juba.
Wakimbizi hao wamekita kambi kwenye ofisi za
umoja wa mataifa baada ya kukimbia mapigano kati ya wanajeshi watiifu kwa Rais Salva Kirr Mayardit na aliyekuwa makamu wake Riek Machar.
Mnamo jumatano wiki hii, kundi la madkatari wasio na mipaka Medecins Sans Frontieres lilisema kuwa watu elfu 20 wanaishi katika hali ya mateso makubwa baada ya mvua iliyonyesha majuzi na kusababisha vyoo kufurika na
kuporomoka.
Toby Lanzer, naibu mkuu wa umoja wa mataifa mjini Juba ameiambia BBC kuwa wanatamaushwa pia na hali mbaya ya maisha ya watu hao waliokimbia mapigano.
Lakini amesema kuwa kambi hiyo ya muda haikuwa ihudumie idadi kubwa ya watu.
Aidha amesema kuwa wanafanya kila wawezalo ili kuboresha sehemu hiyo mbali na kujaribu kukodisha shamba lililo maeneo ya nyanda za juu viungani mwa mji mkuu ili kujenga kambi nyingine ya muda ya kuwahudumia watu.
Umoja wa mataifa wawatelekeza wakimbizi Sudan Kusini
shirika la umoja wa mataifa linalosimamia maswala Sudan UNMISS likipuzilia mbali masaibu yao.
MSF ilitoa picha ya Kambi hiyo ambayo inawatu takriban 21,000 wakiishi katika kambi ambayo maji taka yamezagaa kwote .
Shirika hilo lilitoaushahidi kuwa vyoo 150 vya kambi hiyo vimeporoka na uchafu umetapakaa ovyo.
Zaidi ya watu milioni moja wametoroka makwao .
Takriban watu , 803,200 ni wakimbizi wa ndani kwa ndani huku wengine 254,000 wametorokea nje ya nchi.