Wachezaji wa Bayern Munich wakishangilia moja ya magoli yao dhidi ya Manchester United
Matumaini ya timu ya Manchester
United kufanya maajabu katika ligi ya mabingwa barani Ulaya, UEFA
yaliyeyuka
jana usiku wa Jumatano baada ya kupokea kipigo kutoka kwa
mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Bayern Munich ya Ujerumani cha
magoli 3-1.Hayo yalikuwa ni matokeo ya mchezo wa marudiano baada ya mechi ya kwanza iliyochezwa katika uwanja wa Old Trafford, timu hizo kutoka sare ya magoli 1-1.
Wachezaji wa Manchester United wakishangilia goli
Vijana wa Bayern walizidisha mashambulio katika lango la Manchester United na juhudi zao zilizaa goli katika dakika ya 68 lililofungwa na Tomas Muller.
Arjen Robben alihitimisha safari ya Manchester United baada ya kukwamisha goli la tatu katika dakika ya 76 na kuifanya Bayern Munich kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-2.
UEFA inatarajia kupanga makundi mawili ya timu nne zilizofuzu kucheza hatua ya nusu fainali.
Timu hizo ni Bayern Munich mabingwa watetezi ya Ujerumani walioitoa Manchester United, Atletico Madrid ya Hispania ikiwaondoa Barcelona pia ya Hispania, Real Madrid nayo ikiindoa katika michuano hiyo Borrusia Dortmund ya Ujerumani na Chelsea ya Uingereza ikiisambaratisha PSG ya Ufaransa.