Waandamanaji katika mji mkuu wa Thailand, Bangkok
wameendelea kulenga wizara za serikali, wakidhibiti baadhi ya majengo na
mengine kuyazingira, wakipinga utawala wa waziri mkuu, Yingluck
Shinawatra.
Hati ya kukamatwa imetolewa dhidi ya kiongozi
mmoja wa waandamanaji akihusishwa na hatua ya waandamanaji hao kukalia
majengo ya wizara za serikali.Wakati huo huo bunge la Thailand
linajadili hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu Bi Yingluck.Waandamanaji wanasema wanalenga kukwamisha shughuli za serikali kwa lengo la kumlazimisha waziri mkuu kujiuzulu. Wanasema Bi Yingluck ni kibaraka wa kaka yake, Thaksin Shinawatra ambaye alikuwa waziri mkuu wa zamani wa Thailand aliondolewa madarakani kwa njia ya maandamano.
0 comments:
Post a Comment