Kiongozi wa upinzani wa
Thailand, Yingluck Shinawatra ameshinda katika uchaguzi mkuu, miaka
mitano baada ya kaka yake, Thaksin, kupinduliwa na jeshi.
Waziri Mkuu wa sasa, Abhisit Vejjajiva, amekubali kushindwa.
Wakati wa kampeni vyama vote viwili vilitaka uhasama wa kisiasa ulioleta ghasia nchini humo kwa miaka kadha, umalizike.
Na Thaksin Shinawatra alisema wapigaji kura wa Thailand wamechagua mabadiliko na upatanishi katika taifa.
Akihojiwa na BBC kwa simu kutoka Dubai, ambako anaishi uhamishoni, Bwana Thaksin alisema, hatarudi haraka Thailand: anataka kuchangia katika suluhu siyo matatizo.
Alisema ana hakika kuwa dada yake ana uwezo wa kuongoza nchi.
0 comments:
Post a Comment