MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage amesisitiza kuwa uamuzi wote uliofanywa na kamati ya utendaji ya klabu hiyo ni batili na kwamba hautambui pia uteuzi wa Kocha Zdravko Logarusic wa Croatia.
“Nimeshakwambia kuwa maamuzi yote yalikuwa batili,
kwa sasa sitambui lolote kuhusu huyo Kocha (Logarusic). Mpaka sasa
kocha ninayemtambua ni Abdallah Kibadeni na msaidizi wake Jamhuri
Kihwelo,” alisema Rage.
Rage alisisitiza kuwa kikao hicho kilikuwa ni
batili kwa sababu kilikuwa na lengo la kufanya mapinduzi, hivyo uamuzi
wowote ambao ulifanywa na kikao hicho ni batili.
“Mimi kocha ninayemtambua ni Kibadeni na Julio, huyo mwingine simjui,” alisema Rage jana Jumatatu alipozungumza na Mwanaspoti.
Kamati ya Utendaji ya Simba chini ya makamu
mwenyekiti Joseph Itang’are ilikutana Jumatatu usiku wiki iliyopita na
kumsimamisha Rage aliyekuwa safarini Sudan pamoja na kuliondoa benchi
lote la ufundi chini ya Kibadeni na Julio.
Hiyo ina maana kuwa ujio wa kocha mpya wa Simba,
Logarusic utategemeana na suluhu ambayo inaweza kupatikana baina ya
pande mbili ambazo zinapingana kati ya Rage na Kamati ya Utendaji ya
Simba.
Kibadeni alipoulizwa alisema; “Ni kweli Mwenyekiti
(Rage) amenipigia simu jana (Jumapili) usiku kuniambia kwamba
amenirudisha Simba, sikumkatalia maneno yake siwezi kutoa kauli ya moja
kwa moja hadi nitakapoona kuna taarifa rasmi ya klabu.
“Unajua wakati napewa kazi Simba nilipewa mkataba
pia wakati nasimamishwa kazi hivi juzi pia walinipa barua ambayo
imesainiwa na watendaji wa timu, sasa katika hili nalo natakiwa kupewa
taarifa kwa njia hiyo,kuna muda inabidi utoe nafasi kwa watu wachache
ili wafanye uamuzi wanaouona una manufaa kwao, wao wanadhani mtu
mwingine ataipa Simba ubingwa, basi waendelee naye ili watimize azma
zao,” alisema Kibadeni.
0 comments:
Post a Comment