MBOWE KUPANGUA ‘MAWAZIRI’ WAKE!
- HATIMA YA NAFASI ZA ZITTO KUJULIKANA KARIBUNI
- ALIYEMLALAMIKIA KUHOJIWA POLISI MAKAO MAKUU LEO
Kiongozi wa
Kambi Rasmi Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe,
anatazamiwa kufanya mabadiliko kwa Baraza lake la Mawaziri Kivuli, wakati
wowote katika kipindi cha Mkutano ujao wa Bunge ili kutekeleza maagizo ya
Kamati Kuu iliyokutana hivi karibuni na kumvua wadhifa wake Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Zitto Kabwe.
Zitto
amevuliwa wadhifa wake wa Naibu Katibu Mkuu kutokana na kile kinachodaiwa
anahusika kuandaa waraka wa kufanya mapinduzi ya viongozi ndani ya chama hicho.
Kwa mujibu
wa vyanzo vya habari kutoka ndani ya chama hicho vililiambia gazeti hili kuwa
Kamati Kuu ambayo ndiyo inasimamia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, hivyo mara
baada ya kutangaza kumvua Zitto, wadhifa wake (unaibu katibu mkuu) ilielekezwa
uanze mchakato wa kumuondoa kwenye nafasi zake.
Bungeni,
Zitto ni Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi akiwa msaidizi wa Mbowe na Waziri Kivuli
wa
Wizara
ya Fedha. " Kwa nafasi yake ndiye alikuwa akishiriki kuandaa bajeti ya
upinzani bungeni, kuwasilisha bajeti ya wizara ya fedha akiwa waziri kivuli,
lakini kwa kuvuliwa wadhifa wake maana yake haaminiki tena," alisema mmoja
wa watoa habari ndani ya chama hicho kwa sharti la jina lake kutochapishwa
gazetini.
Hata hivyo, juhudi za kumpata Mkurugenzi wa Habari na
Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, ili kuweza kuzungumzia suala hilo ziligonga mwamba kutokana na simu yake
ya kiganjani kutopokelewa.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Makao Makuu jijini Dar es Salaam leo linatarajia kufanya mahojiano na Katibu
wa CHADEMA mkoa wa Dar es Salaam,
Henry Kileo, baada ya mahojiano hayo kukwama kufanyika jana kutokana na
malalamiko yanayodaiwa kuwasilishwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
Mahojiano hayo yalikuwa yafanyike Makao Makuu ya Jeshi la Polisi
jijini Dar es Salaam jana mchana, lakini yaliahirishwa muda mfupi baada ya
Kileo kuwasili akiwa na mwanasheria wake na makada wengine wa CHADEMA.
Baada ya kufika maofisa wa Polisi walifanya mazungumzo na
mwanasheria wake, lakini baada ya muda walikubaliana yafanyike leo saa tano.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kileo, alisema awali mahojiano
yalitakiwa yafanyike jana saa nane mchana, lakini walichelewa kufika makao
makuu ya polisi kutokana na wakili wake kuchelewa kwani alikuwa na kesi makao
makuu ya Polisi.
Kileo, alipoulizwa anatakiwa polisi kwa ajili ya makosa gani,
alisema hana taarifa kwa undani, kwani alipigiwa simu na ofisa
aliyejitambulisha kwa jina la Mbutta na kumwambia kuwa anatakiwa kufika makao
makuu ya Polisi kwa mahojiano kutokana na malalamiko ambayo Zitto,
ameyafikisha.
"Niliambiwa nahitajika kujibu tuhuma ambazo Zitto
amezifikisha Polisi, lakini sikuelezwa ni tuhuma gani hizo," alisema
Kileo. Alipoulizwa ni kwa nini Zitto apeleke shtaka hilo
Makao Makuu ya Polisi, badala ya vituo vingine kama ilivyo kawaida, Kilewo
alijibu; "Mimi sijui labda wapigie polisi ili muwaulize swali hilo."
Gazeti moja (sio
Majira) jana lilichapisha habari inayoeleza kuwa Zitto, amemfungulia mashtaka
Kileo akimtuhumu kusambaza waraka katika mitandao ya kijamii unaomhusisha na
mipango ya kufanya mapinduzi ya chama hicho

0 comments:
Post a Comment