
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), DK Joyce Ndalichako (kulia) akizungumza baada ya kupata maelezo ya namna teknolojia mpya ya kusahihisha maswali ya kujieleza inavyofanya kazi. Wengine ni maofisa wa Kampuni ya DRS iliyobuni teknolojia hiyo. Picha na Fredy Azzah
Mwaka jana Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), lilianza kutumia teknolojia mpya ya usahihishaji wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi.
Kabla ya matumizi ya teknolojia hiyo inayotumia kompyuta (Optical Mark Reader), baraza lilisema teknolojia hiyo ingesaidia kupunguza muda pamoja na gharama za usahihishaji.
Ilisema pia teknolojia hiyo, ingetoa fursa ya wanafunzi kupimwa kwenye nyanja mbalimbali walizofundishwa na pia kuongeza umakini katika kusahihisha mitihani.
Ili kuweza kutumika kwa teknolojia hiyo wanafunzi walipaswa kutumia karatasi maalu mu za kujibia mitihani, zilizosahihishwa na mashine ya OMR, ambayo pamoja na mambo mengine pia huonyesha maswali yaliyojibiwa vizuri na yale yenye changamoto.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Joyce Ndalichako anasema kuwa matumizi ya OMR mbali na kupunguza gharama za usahihishaji na kuharakisha shughuli hiyo, yamesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza makosa yaliyokuwa yakifanyika wakati wa kusahihisha mitihani hiyo kwa kutumia mikono.
“Baada ya kufanya tathmini ya mfumo huu kwa mwaka jana, tumebaini kuwa mashine haikufanya kosa hata moja. Baadhi ya makosa yaliyojitokeza yalisababishwa na watu na mashine iliwaumbua,” anasema na kuongeza:
“Watu wanasema kuwa mtihani wa maswali ya kuchagua ni rahisi, lakini siyo kweli, inatungwa na wataalamu na unalenga kumpima mtoto katika kila nyanja. Ndiyo maana hata mtihani wa darasa la saba mwaka jana ilibidi Serikali ishushe alama za kwenda kidato cha kwanza zikawa 70 badala ya 100.”
Anasema kwa kidato cha nne na kuendelea, wameweka mfumo ambao baada ya kumaliza kusahihisha, mhusika anaingiza alama zake kwenye mfumo ambao hakuna mtu anayeweza kuubadilisha.
“Zikishaingizwa kwenye mfumo kutoka kwenye kituo cha usahihishaji, hakuna mtu anayeweza kuzigusa na akigusa anaonekana. Hata msahihishaji akishaziweka mara moja hawezi kuzigusa tena na hakigusa anaonekana. Kwa hiyo kwa mfumo huu huwezi kumuongezea mwanafunzi alama,” anabainisha.
Teknolojia ya maswali ya kujieleza
0 comments:
Post a Comment