Arsene Wenger aendelee au asiendelee?
Ndio wimbo unaorindima ndani ya mioyo ya mashabiki wa Arsenal.Mashabiki wanamlaumu Wenger naye Wenger mwenyewe anakilaumu kikosi chake.
"Lililobaki kwa silimia 100 tutang'ang'ania nafasi ya nne ingawaje ni vigumu," Wenger amesema.
Shabiki mmoja auliza katika mtandao wa twitter kuwa iweje January walikuwa nambari moja, february nambari 2, Mwezi wa tatu 3 na sasa mwezi wa nne nambari nne?
Mashabiki wamtaka wenger ajiuzulu
Amejiunga na wale ambao wameanzisha kampeni katika mtandao Wenger ajiuzulu.
Kilio cha Arsenal ni furaha ya Liverpool ambao baada ya kuitandika West ham 2-1 wametuliza kileleni mwa ligi
Bashasha sasa pia zasikika katika kambi iliyokuwa imefifia ya Manchester United baada ya kuimwagia machungu yao yote Newcastle 4- 0 .
Kutokana na Ushindi huo Vijana wa David Moyes hatimaye wameimarika kutoka nafasi ya 7 hadi nambari 6.

0 comments:
Post a Comment