Taarifa
kutoka mkoani Singida zinasema kuwa Lori la mafuta limeanguka jioni ya
February 19 katika eneo la milima ya sekenke na kuua watu wanne
hapohapo.
Chanzo cha ajali hiyo ni inasemekana ni kufeli kwa
breki wakati lori hilo lilipokuwa linashuka mlima huo,miongoni mwa
mashuhuda wa ajali hiyo Bwana Julius Chacha alipoongea na mtandao Dj sek
blog na kusema Lori hilo lilipoacha njia lilipinduka na kuingia
bondeni.
Mara baada ya kuingia bondeni Lori hilo lilishika moto
na mashuhuda hao walishindwa kutoa msaada wowote kwa kwa moto uliposhika
ulikuwa mkubwa na hawakuwa na vifaa vya kuokolea.
Taarifa mpaka
sasa inasema Watu wanne wamekuufa papo hapo kutokana na ajali
hiyo,mashuhuda wanadai polisi walichelewa kufika eneo la tukio