skip to main |
skip to sidebar
Kazi
ya kwanza nilifanya Bungeni ilikuwa ni kuhesabu kura za kumthibitisha
Waziri Mkuu Edward Ngoyai Lowasa. Spika Samwel Sitta aliteua mbunge
mwenye umri mdogo zaidi na mbunge wa kuchaguliwa mwenye umri zaidi.
Amina Chifupa na mie tulienda kuhesabu kura zile. Kura 3
ziliharibika.
Karani wa Bunge akatuomba tusirekodi kura zilizoharibika kwani ni aibu
kwa wabunge. Amina akakataa kwa kusema "aibu gani,
wananchi wawajue wabunge wao"! Nilishikwa butwaa. Wakati huo watu wengi
walimdharau mbunge huyu kama 'mtangazaji' tu tena wa mipasho. Jioni ya
siku ile Disemba 29, 2005 ilibadili kabisa mtazamo wangu kuhusu watu na
uwezo wao. Amina alishangaza wengi kiuwezo hasa vita yake dhidi ya dawa
za kulevya.
0 comments:
Post a Comment